Chunusi ni viuvimbe vidogo vinavyojitokeza usoni kushuka kifuani ,sehem za kwenye mabega na mgongoni. kwa sababu maeneo hayo yana vishimo vidogo vya kupitisha jasho kwenye ngozi ambavyo huzibwa na mafuta au viseli vya ngozi zilizokufa(Dead skin cells) au hutafunwa na wadudu(Bacteria) na kusababisha vimbe hizo.
kitaalam chunusi huitwa ACNE VULGARIS na huwapata sanasana vijana wakati wa kipindi cha kubalehe /kuvunja ungo(Adolescence period) karibu 80% ya vijana kati ya umri kuanzia miaka 14-25 hupata vimbe hizi(chunusi) na karibu 25% ya wanawake wenye umri kati ya miaka 21 hupata chunusi.
Chunusi hizi hushambulia sana vifuko vya ngozi(Sebaceous Glands) zipatikanazo chini ya ngozi ambavyo hutoa mafutamafuta yaitwayo Sebum yasaidiayo kuifanya ngozi iwe na unyevu unyevu na kuongeza mvuto wake, Sebum hujitokeza kwa wingi wakati wa kubalehe hvyo huzalisha homon nyingi za jinsia(sex hormone) hasa za kiume ziitwazo Androgens zinazoungana na seli mfu za ngozi na kutengeneza mchanganyiko mzito mfano wa gundi au nta ijulikanayo kama Comedo inayoziba vishimo vya kutolea jasho na joto
Maambukizi huongezeka maradufu pale backteria wanaposhambulia vishimo vilivyoziba na kusababisha vimbe kubwa zaidi ya awali zijulikanazo kama chunusi kubwa (Pimples) ambazo hutokana na mchanganyiko mkubwa wa sebum,bakteria,seli mfu za ngozi pamoja na seli hai nyeupe za damu katika vishimo vya jasho vilivyoziba.

CHANZO CHA CHUNUSI
kunaviashiria mbali mbali ambavyo huonekana kama visababishi vya kutokea kwa chunusi ambavyo ni..
1. UMRI – Kama nilivyosema hormone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubalehe.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta/gundi (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
2. VIPODOZI –Baadhi ya vipodozi kama Make-up za kike na Sprays za nywele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
3. CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na vyakula moja kwa moja ila vyakula vyenye mafuta mafuta(Fat) na Protein vimekuwa kama vichocheo vya kuongeza chunusi.
4. DAWA- Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na makusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
5. MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana. pia Magonjwa ya allergy yatokanayo na mzio wa vyakula.
6. MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi au hewa chafu,sehem zenye uvundo huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
7. JINSIA-Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana kwasababu hormone za uzazi ziitwazo Testosterone huongezeka kwa wingi zaidi.
8. HOMONI- Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkubwa hupelekea kupata chunusi.
9. USAFI MWILINI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa au kuzitumbua chunusi au vipele husababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwilini au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
KUJUA JINSI YA KUEPUKANA NA CHANGAMOTO HII SUGU. NAPATIKANA KWA NAMBA ZIFUATAZO:
0715280233
0769280233
0625738210
0715280233
0769280233
0625738210
Whatsapp number 0715 280 233
source;IFAKARA YETU